NEWS

Mambo 10 Usiyoyajua Kuhusu Wanawake Au Wasichana.

Unaweza ukajiisi labda ni mwenye bahati sana na mwenye kujua kwa kujihisi labda unafahamu sana kuhusiana na wanawake lakini jibu ni unachokijua ni theluthi tu na umebakisha mambo lukuki ambayo unatakiwa kuyajua kwasababu kila siku wanazaliwa na tabia zipo za kila aina na zinatofautiana.
Nimekuandalia mambo 10 tafauti kuhusiana na wanawake ambayo ulikuwa hauyafahamu na ni vyema kuyafahamu kwa wakati huu maybe yataweza kukusaidia kwa wakati huu au hata baadaye.
1. KUHUSU TAMAA ZAO.
Mwanamke yeyote anaweza kukutamani kimapenzi isipokuwa Mama yako.
2. KUHUSU HULKA ZAO.
Wanawake wote huonesha upendo wao waziwazi isipokuwa wale waliotendwa kabla.
3.KUHUSU KUACHANA.
Mwanaume kumuacha mwanamke anayempenda ni kama simba kuacha kula swala, Mwanamke kumuacha mwanaume ni rahisi kama swala kumkimbia Simba mzee.
4.KUHUSU TABIA.
Jihadhari na maneno ya vijiweni kwamba wanawake wote wako sawa kitabia. No, lakini kumbuka hakuna Mwanamke asie Mwanamke.
5. KUHUSU MPENZI WA ZAMANI.
Mwanamke kujaribu kumsahau mwanaume aliyewahi kumpenda Ni ngumu.
6. KUHUSU KUOLEWA.
Muhimu kuoa, na ni ngumu sana Kumjua mke mwema kabla ya kuoa, ni waigizaji wazuri sana. Kumbuka maneno haya” Muhimu kuoa, ukipata mke mwema utakuwa na furaha, ukipata mke mwovu utakuwa mwanafalsafa.
7. KUHUSU USALITI.
Vizuri kujiandaa kisaikolojia kusalitiwa, ila usipojiandaa  waweza kuua mtu au hata kujiua. ukiua mtu maisha yako yatakosa furaha siku zote, ukijiua mwenyewe, hao waliokusaliti wanaweza kuishi kwa furaha zaidi ya ulivyokuwa hai.
8.KUHUSU PESA NA MAPENZI.
Mapenzi bila pesa yanapatikana kwa wingi sana huko mbinguni, hapa duniani ni ngumu mno, lakini usihofu sana, kuna makubaliano bila pesa. Omba MUNGU.
9. KUHUSU UONGO.
Wahenga walisema Ukweli unauma, Na mimi nakuambia “Uongo unaua”
10. KUHUSU KUWAJUA WANAWAKE.
Kijana, Kutaka kumjua mwanamke unahitaji miaka mingi ya kuishi kuliko idadi ya nywele zao. Usihangaike na vitabu, makala, majarida, filamu, nyimbo na hotuba za wanaofundisha mandhari za wanawake. Kuna kanuni moja tu ya kupenda, “ili ubaki salama katika kupenda sharti ujipende kwanza”.